Mark 1:29-34

29 aMara walipotoka katika sinagogi, walikwenda pamoja na Yakobo na Yohana hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea. 30Mama mkwe wa Simoni alikuwa kitandani, ana homa, nao wakamweleza Isa habari zake. 31 bHivyo Isa akamwendea, akamshika mkono na kumwinua. Kisha homa ikamwacha, naye akaanza kuwahudumia.

Isa Aponya Wengi

(Mathayo 8:16-17; Luka 4:40-41)

32 cJioni ile baada ya jua kutua, watu wakamletea Isa wagonjwa wote na waliopagawa na pepo wachafu. 33Mji wote ukakusanyika mbele ya nyumba hiyo. 34 dIsa akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Akawatoa pepo wachafu wengi, lakini hakuwaacha hao pepo wachafu waseme, kwa sababu walimjua yeye ni nani.

Isa Aenda Galilaya

(Luka 4:42-44)

Copyright information for SwhKC